sw_tw/bible/other/sacrifice.md

879 B

dhabihu, sadaka

Ufafanuzi

Katika Biblia, maneno "dhabihu" na "sadaka" ya husu zawadi maalumu anazopewa Mungu kama kitendo cha kumuabudu. Watu pia walitoa sadaka kwa miungu ya uongo.

  • Neno "sadaka" la husu chochote kinacho tolewa au kupewa. Neno "dhabihu" la husu kitu kinacho tolewa au kufanywa kwa gharama kubwa kwa mtoaji.
  • Sadaka kwa Mungu zilikuwa vitu maalumu alizo waamuru Waisraeli kutoa ili kuonyesha upendo na utii kwake.
  • Maneno ya sadaka tofauti, kama "sadaka ya kuteketeza" na "sadaka ya amani," ili hashiria aina gani ya sadaka ilitolewa.
  • Dhabihu kwa Mungu kulihusisha kuua mnyama.
  • Dhabihu peke yake ya Yesu, Mwana mkamilifu, asiye na dhambi, wa Mungu, anaweza kutakasa watu na dhambi. Mnyama hakuweza kufanya hivyo.
  • Mfano wa msemo "jitoeni kama dhabihu hai" ina maana, "ishi maisha yako kwa kumtii Mungu, kuacha kila kitu ili kuweza kumtumikia.