sw_tw/bible/other/purple.md

672 B

Zambarau

Ufafanuzi

Hii ni rangi ambayo ni mchanganyiko kati ya rangu ya bluu na nyekundu.

  • Hapo kale rangi ya zambarau ilikuwa hadimu na ya thamani sana ilitumika kama vazi kwa wafalme na viongozi wakuu.
  • Kwa sababu ilikuwa ya gharama na ilichukua muda kutengeneza vazi la rangi ya zambarau ilikuwa alama ya utajiri na ufalme.
  • Pia zambarau ilikuwa rangi iliyotumika kwenye mapazia ya hekalu na nguo zilizovaliwa na makuhani.
  • Askari wa Rumi walimvalisha Yesu vazi la zambarau kabla hawajamsulubisha ili kumdhihaki kwa kuwa alisema yeye ni mfalme wa Wayahudi.
  • Lidia toka katika mji wa Filipi alikuwa mwanamke aliyejipatia kipato kwa kuuza nguo za zambarau.