sw_tw/bible/other/possess.md

11 lines
586 B
Markdown

# Kumiliki, Miliki
## Ufafanuzi
"Kumiliki" au "miliki" ni kitendo cha kuwa na kitu fulani. Pia inaweza kuwa na maana ya kuwa na mamlaka juu ya kitu fulani au kumiliki eneo la ardhi.
* Katika agano la kale neno hili limetumika kama kumiliki ardhi katika eneo.
* Bwana alipowaamuru Waisraeli wamiliki nchi ya Kanaani inamaanisha kuwa walitakiwa kwenda kwenye nchi ile na kukaa huko. Hii inajumuisha kuwashinda watu wa Kanaani waliokuwa wakiishi huko.
* Bwana aliwaambia Waisraeli kwamba amewapa nchi ya Kanaani kama milki yao. Hii inaweza kutafsiriwa kama "sehemu sahihi ya kuishi."