sw_tw/bible/other/pomegranate.md

472 B

Komamanga

Ufafanuzi

Komamanga ni aina ya tunda nene lenye ngozi ngumu lililojaa mbegu nyingi ndani zilizozungukwa na chakula chenye rangi nyekundu.

  • Komamanga mara nyingi huota katika nchi zenye joto, ukame kama Miisri na Israeli.
  • Bwana aliwaahidi wa Israeli kuwa Kanaani ni chi yenye maji ya kutosha na ardhi yenye rutuba iliyo na vyakula vya kutosha ikiwemo makomamanga.
  • Ujenzi wa hekalu la Sulemani lilikuwa na mapambo yaliyo katika muundo wa komamanga.