sw_tw/bible/other/peaceoffering.md

612 B

Sadaka ya amani.

Ufafanuzi

Sadaka ya amani ilikuwa moja ya sadaka ambayo Mungu aliwaamuru Waisraeli watoe. Mara nyingine iliitwa sadaka ya shukrani au sadaka ya ushirika.

  • Sadaka hii inajumuisha kutoa mnyama asiye na kasoro na kuinyunyuzia damu ya myama katika madhabahi na kuteketeza mafuta ya mnyama pamoja na vipande vya mnyama vilivyobaki kwa kutenganisha.
  • Katika sadaka hii iliambatana na mkate wenye chachu na usiotiwa chachu ambayo iliteketezwa juu ya sadaka.
  • Kuhani na mtoa sadaka waliruhusiwa kula chakula kilichotolewa kama sadaka.
  • Sadaka hii ilionesha ushirika wa Mungu na watu wake.