658 B
658 B
Ng'ombe, fahali, ndama, mifugo
Ufafanuzi
Mifugo ni kundi kubwa la wanyama wenye miguu minne wanaokula majani na hufugwa kwa ajili ya maziwa na nyama.
- Ng'ombe dume huitwa fahali na ng'ombe mdogo huitwa ndama.
- Mara nyingine ng'ombe hutumika kuwakilisha aina zote za mifugo.
- Katika tamaduni zingine ng'ombe hubadilishwa na bidhaa katika biashara. Mara nyingine hutumika kama zawadi itolewayo kwa wazazi wa binti na mwanaume anayetaka kumuoa.
- Katika Biblia Wayahudi walitumia mifugo kwa ajili ya dhabihu hasa ng'ombe mwekundu.
- Ng'ombe mwekundu ni ng'ombe ambaye hajazaa bado.
- Pia kuna ng'ombe dume ambaye hutumika katika shughuli za kilimo.