sw_tw/bible/other/council.md

746 B

Halmashauri

Ufafanuzi

Halmashauri ni kundi la watu wanaokutana kujadili, kutoa ushauri na kufanya maamuzi juu ya masuala ya muhimu.

  • Halmashauri huratibiwa kwa namna maalumu kwa ajili ya lengo fulani kwa mfano kufanya maamuzi juu ya masuala ya kisheria.
  • "Halmashauri ya kiyahudi" katika Yerusalemu inayojulikana kama "Baraza" lilikuwa na wajumbe 70 wakiwemo viongozi wa kiyahudi, kuhani mkuu, waandishi, mafarisayo na masadukayo waliokusanyika mara kwa mara kuamua mambo ya sheria za Kiyahudi. Halmashauri hii ya viongozi wa dini iliyomuweka Yesu kwenye mashtaka na kuamua auawe.
  • Pia kulikuwa na halmashauri ndogo za Kiyahudi katika miji mingine.
  • Mtume Paulo alipelekwa mbele ya halmashauri ya Rumi alipokamatwa akihubiri injili.