sw_tw/bible/other/cherubim.md

862 B

Makerubi, Kerubi

Ufafanuzi

Kerubi ni umoja na makerubi ni wingi. Hivi ni viumbe vya pekee vya mbinguni alivyoviumba Mungu. Biblia inawaelezea makerubi kuwa wana mabawa na moto.

  • Makerubi wanadhihirisha utukufu na nguvu za Mungu na pia ni walinzi wa vitu vitakatifu.
  • Baada ya Adamu na Eva kutenda dhambi Mungu aliweka makerubi wenye upanga wa moto katika upande wa mashariki mwa bustani ya Edeni ili mtu yeyote asiweze kuupata mti wa uzima.
  • Mungu aliwaamuru Waisraeli kuchonga makerubi wawili wanaoangaliana mabawa yao yakiwa yamegusana kwenye mfuniko wa upatanisho wa sanduku la agano.
  • Pia aliwaambia wafume picha za makerubi katika mapazia ya maskani.
  • Katika vifungu vingine viumbe hawa wameelezewa kuwa na nyuso nne, ya mtu, simba, ng'ombe na malaika.
  • Makerubi wakati mwingine wanadhaniwa kuwa ni malaika japokuwa Biblia haijaeleza hivyo.