sw_tw/bible/other/burden.md

809 B

mzigo

Ufafanuzi

Mzigo ni kitu kizito. Kwa uhalisia inamaanisha uzito wa kitu ambacho mnyama wa kazi angeweza kubeba. Neno "mzigo" pia linamaana kadhaa za kimafumbo:

  • Mzigo waweza kumaanisha kazi ngumu au wajibu wa mhimu ambao mtu anapaswa kuufanya. Anaswemwa "kuuchukua" au "kuubeba" "mzigo mzito."
  • Kiongozi katili aweza kuweka mizigo mizito kwa watu anaowaongoza, mfano kwa kuwalazimisha kulipa kiwango kikubwa cha ushuru.
  • Mtu asiyependa kuwa mzigo kwa mtu mwingine hapendi kumsababishia mtu huyo shida yoyote.
  • Hatia ya dhambi za mtu ni mzigo kwake.
  • "Mzigo wa Bwana" ni tamathari ya usemi kumaanisha "ujumbe kutoka kwa Mungu" ambao nabii anapaswa kuutoa kwa watu wa Mungu.
  • Neno "mzigo" laweza kufasiriwa kuwa "wajibu" au "jukumu" au "mzigo mzito" au"ujumbe," kutegemeana na mazingira.