668 B
668 B
shaba
Ufafanuzi
Neno "shaba" linamaanisha aina ya madini yatengenezwayo kwa kuyeyusha kwa pamoja metali, shaba nyekundu na bati. Ina rangi nyeusi inayoelekea njano, nyekundu kiasi.
- Shaba huzuia kutu na kipitisho kizuri cha joto
- Hapo kale, shaba ilitumika kutengeneza dhana, silaha, madhabahu, vyungu, silaha za askari na vitu vingine.
- Vifaa vingi vya kujengea hema la kukutania na hekalu vilikuwa vimetengenezwa kwa shaba.
- Kwa kawaida vinyago vya miungu ya uongo vilitengenezwa kwa madini ya shaba.
- Dhana za shaba zilitengenezwa baada ya kuyeyusha madini ya shaba na kisha kuyamimina katika chombo cha kutengenezea. Mchakato huu uliitwa "kutupa."