sw_tw/bible/other/bold.md

784 B

jasiri, ujasiri, ushujaa

Ufafanuzi

Maneno yote haya yanamaanisha kuwa na ujasiri na ushujaa kwa kuongea ukweli kuhusu jambo halali hata kama ni vigumu na hatari.

  • Mtu "jasiri" haogopi kusema jambo jema na la haki, ikiwa ni pamoja na kuwatetea watu wanaonyanyaswa. Hii yaweza kufasiriwa kama "ujasiri" au "bila hofu".
  • Katika Agano Jipya, wanafunzi waliendelea kuhubiri kwa "ujasiri" kuhusu Kristo hadharani, bila kujari hatari ya kufungwa au kuuawa. Hii inatafasiriwa kama "ujasiri" au "ushujaa" au "kwa ujasiri."
  • "Ujasiri" wa wanafunzi hawa wa mwanzo katika kuhubiri habari njema ya kifo kiokoacho cha Kristo msalabani kilisababisha injili kuenea katika Israeli yote na nchi za jirani na hatimaye, katika dunia yote. "Ujasiri" waweza pia kutafasiriwa kama "ushujaa."