803 B
803 B
kufuta
Ufafanuzi
Maneno "kufuta" au "kuondoa" ni vifungu vinavyomaanisha kuondoa kabisa au kuangamisa kitu au mtu.
- Vifungu hivi vyaweza kutumika katika maana chanya, kama ambavyo Mungu "hufuta" dhambi kwa kusamehe na kuchagua kutokukumbuka tena.
- Lakini pia yaweza kutumika katika maana mbaya, kama ambavyo Mungu "hufuta" au "kuondoa" kundi la watu, kuwaharibu kwa sababu ya dhambi.
- Biblia inazungumzia juu ya jina la mtu "kufutwa" au "kuondolewa" katika kitabu cha Mungu, kumaanisha mtu hatapokea uzima wa milele.
Maone ya Kutafasiri
- Kwa kutegemea mazingira, vifungu hivi vyaweza kutafasiriwa kama "kuondoa" au "kutoa" au " kuharibu kabisa" au "kuondoa kabisa."
- Kwa kurejerea kufuta jina la mtu katika Kitabu cha Uzima, yaweza kutafasiriwa kama "kuondoa kutoka" au "iliyofutwa."