sw_tw/bible/other/bloodshed.md

1.1 KiB

kumwaga damu

Ufafanuzi

Neno "kumwaga damu" linamaanisha kifo cha mwanadamu kwa sababu ya mauaji, vita, au sababu nyingine ya kikatiri.

  • Neno hili "kumwaga damu," kwa kawaida linamaanisha wakati damu inapotoka katika jeraha katika mwili wa mtu.
  • Neno "kumwaga damu" linatumika mara kwa mara kurejerea mauaji ya watu yaliyoenea.
  • Lakini pia linatumika kama kumbukumbu ya jumla kwa dhambi ya kuuwa.

Maoni ya Kutafasiri

  • "Kumwaga damu" kwaweza kutafasiriwa kama, "mauaji ya watu" au "watu wengi waliouawa".
  • "Kupitia umwagaji wa damu" yaweza pia kutafasiriwa kama, "kwa kuuwa watu."
  • "Kumwaga damu ya wasio na hatia" yaweza kutafasiriwa kama "kuuwa watu wasio na hatia".
  • "Kumwaga damu kunafuata kumwaga damu" kwaweza kutafasiriwa kama, "wanaendelea kuuwa watu" au "kuuawa kwa watu kunaendelea" au "wameua watu wengi na wanaendelea kufanya hivyo" au "watu wanaendelea kuuwa wengine."
  • Matumizi mengine ya tamathari, "kumwaga damu kutakufuata" kwaweza kutafasiriwa kama "watu wako wataendelea kushuudia mauaji" au "watu wako wataendelea kuuawa" au "watu wako wataendelea kuwa katika vita na mataifa mengine na watu wataendelea kufa.