sw_tw/bible/other/biblicaltimeyear.md

931 B

mwaka linapotumika

Ufafanuzi

Neno "mwaka linapotumika, kwa hali ya kawaida katika Biblia linamaanisha kipindi cha muda wa siku 354. Hii ni kulingana na kalenda inayotumia mfumo wa mwezi unaochukua kuizunguka dunia.

  • Mwaka katika siku hizi unakamilisha siku 365 kwa kugawanywa katika miezi 12, kutegemea siku ambazo dunia inatumia kulizunguka jua.
  • Katika mifumo yote miwili mwaka una miezi 12. Lakini wakati mwingine ziada ya mwezi wa 13 unaongezwa katika mwaka unaotumia kalenda ya mwezi kwa kuzingatia kuwa kalenda ya mwezi ina siku 11 pungufu ya ule wa jua. Hii inasaidia kuzilinganisha kalenda zote mbili.
  • Katika Biblia, neno "mwaka" pia limetumika kwa tamathari kuonesha muda wa jumla tukio maalumu linapotokea. Mfano wake ni "mwaka wa Yahwe" au "katika mwaka wa kianganzi" au "mwaka wa Bwana uliokubarika." Katika mazingira haya, "mwaka" waweza kutafasiriwa kama "wakati" au "majira" au "kipindi cha wakati".