sw_tw/bible/other/biblicaltimehour.md

14 lines
1.0 KiB
Markdown

# saa
## Ufafanuzi
Neno "saa" linatumika mara kwa mara katika Biblia kuonesha muda wa siku jambo fulani lilipotendeka. Pia linatumia tamathari kumaanisha "wakati" au "kitambo"
* Wayahudi walihesabu masaa ya kutwa kuanzia mawio ya jua (kama saa 12:00 asubuhi). Kwa mfano, "saa tisa" alasiri.
* Masaa ya usiku yalihesabiwa kuanzia machweo (kama saa 12: 00 jioni). Kwa mfano, "saa tatu ya usiku" kumaanisha karibia saa tisa za usiku" katika mfumo wetu wa siku hizi.
* Kwa kuwa kumbukumbu za muda katika Biblia hazitalingana kamili na mfumu wa siku hizi, vifungu kama vile "karibia saa tisa" au "kama saa sita kamili" yaweza kutumika.
* Baadhi ya tafasiri zaweza kuonesha vifungu kama vile "wakati wa jioni" au "wakati wa asubuhi" au "wakati wa mchana" kuweka wazi ni muda upi wa siku unaozungumzwa.
* Kirai, "wakati uo" chaweza kutafasiriwa kama "katika wakati ule" au "katika kitambo hicho".
* Kwa kumtaja Yesu, kifungu "wakati wake umefika" yaweza kutafasiriwa kama, "muda wake wa kufanya" au "muda uliowekwa kwa ajili yake ulikuwa umefika."