sw_tw/bible/other/believer.md

909 B

mwamini

Ufafanuzi

Katika Biblia, neno "mwamini" larejerea mtu anayeamini na kumtegemea Yesu Kristo kama Mwokozi.

  • Neno "mwamini" kwa maana halisi linamaanisha "mtu anayeamini."
  • Neno "Mkristo" lilikuja hatimaye kuwa jina la waamini kwa sababu linaonesha kwamba wanamwamini Kristo na kutii mafundisho yake.

Maoni ya Kutafasiri.

  • Baadhi ya tafasiri zaweza kupendelea kusema, "mwamini wa Yesu" au "anayemwamini Kristo."
  • Neno hili pia laweza kufasiriwa kwa neno au kirai kinachomaanisha, "mtu anaye mwamini Yesu" au "mtu anayemfahamu Yesu na kuishi kwa ajili yake."
  • Njia nyingine ya kutafasiri "mwamini" laweza kuwa, "mfuasi wa Yesu" au "Mtu anayemjua na kumtii Yesu."
  • Neno "mwamini" ni neno la jumla kwa kila anayemwamini Kristo, wakati "mfuasi" na "mtume" yalitumika maalumu kwa watu waliomfahamu Yesu alipokuwa hai. Ni vema kutafasiri maneno haya kwa njia tofauti, ili kuyatofautisha.