sw_tw/bible/other/ambassador.md

501 B

Balozi, mwakilishi

Ufafanuzi

Balozi ni mtu aliyechaguliwa rasmi kuwakilisha nchi yake katika mataifa ya kigeni. Mara nyingine hutafsiriwa kama mwakilishi.

  • Balozi au mwakilishi huwapa watu ujumbe aliopewa na mtu au serikali iliyomtuma.
  • "Mwakilishi" ni yule aliyepewa mamlaka ya kufanya au kuzungumza kwa niaba ya yule anayemwakilisha.
  • Mtume Paulo anawafundisha Wakristo kuwa ni mabalozi wa Kristo au wawakilishi kwa kuwa wanamwakilisha Kristo duniani na kuwafundisha wengine ujumbe huu.