sw_tw/bible/names/zechariahot.md

782 B

Zakaria

Ufafanuzi

Zakaria alikuwa nabii aliyetabiri wakati wa utawala wa Mfalme Dario I wa Uajemi. Kitabu cha Zakari katika Agano la Kale kina unabii wake, ambacho kinawasihi mateka waliorudi kulijenga tena hekalu.

  • Nabii Zakaria aliishi wakati mmoja na Ezra, Nehemia, Zerubabeli na Hagai. Alitajwa na Yesu kama nabii wa mwisho kati ya wale waliouawa katika nyakati za Agano la Kale.
  • Mtu mwingine mwenye jina la Zakaria alikuwa bawabu katika hekalu wakati wa Daudi.
  • Mmoja wa wana wa Mfalme Yehoshafati aliyeitwa Zakaria aliuliwa na Yehoramu nduguye.
  • Zakaria alikuwa kuhani aliyeuawa kwa kupigwa mawe na watu wa Israeli alipowakemea kwa ibada yao ya sanamu.
  • Mfalme Zakaria alikuwa mwana wa Yeroboamu na alimiliki juu ya Israeli kwa miezi sita tu kable ya kuuawa.