862 B
862 B
Stefano
Ufafanuzi
Stefano anajulikana kama Mkristo wa kwanza kuuawa, sababu ya imani yake kwa Yesu. Maisha yake na kifo yameandikwa kwenye kitabu cha Matendo.
- Stefano alichaguliwa na Kanisa la awali la Yerusalemu kutumikia Wakristo kama shemasi kuwapa chakula wajane na wengine Wakristo wenye maitaji.
- Baadhi ya Wayahudi walimshtumu kwa uongo Stefano kuzungumza dhidi ya Mungu na dhidi ya sheria ya Musa.
- Stefano kwa ujasiri alisema ukweli kuhusu Yesu Mesiya, kwa kuanza na historia ya matendo ya Mungu kwa Waisraeli.
- Viongozi wa Wayahudi walikasirika na kumuua Stefano kwa kumpiga mawe hadi kufa nje ya mji.
- Kifo chake kilishuhudiwa na Sauli wa Tarso, baade kuwa mtume Paulo.
- Stefano anajulikana pia kwa maneno yake ya mwisho kabla ya kufa: Bwana, tafadhali usihesabu dhambi hii dhidi yao," iliyo onyesha upendo aliyo kuwa nao kwa wengine.