sw_tw/bible/names/rahab.md

11 lines
371 B
Markdown

# Rahabu
## Ufafanuzi
Rahabu alikuwa mwanamke aliyeishi Yeriko Waisraeli walipovamia mji. Alikuwa kahaba.
* Rahabu aliwaficha Waisraeli wawili waliokuja kupeleleza Yeriko kabla ya Waisraeli kuvamia. Aliwasaidia wapelelezi kurudi kwenye kambi ya Israeli.
* Rahabu akamwamini Bwana.
* Yeye na familia yake hawakudhuriwa Yeriko ilipoharibiwa na wakaenda kuishi Israeli.