667 B
667 B
Finehasi
Ufafanuzi
Finehasi ni jina la watu wawili katika agano la kale.
- Mmoja wa wajukuu wa Haruni alikuwa kuhani aliyeitwa finehasi aliyepinga kwa nguvu kuabudu miungu ya uongo.
- Finehasi aliwaokoa Waisraeli toka kwenye pigo ambalo bwana alilituma ili kuwaadhibu kwa kuwaoa wanawake wa Midiani na kuabudu miungu yao ya uongo.
- Katika matukio mbali mbali Finehasi alikwenda na jeshi la Israeli kuwapiga Wamidiani.
- Finehasi mwingine aliyetajwa kwenye agano la kale alikuwa mmoja wa wana waovu wa kuhani Eli katika kipindi cha nabii Samweli.
- Finehasi na kaka yake Hofini waliuawa kipindi ambacho Wafilisti walivamia Israeli na kuiba sanduku la agano.