561 B
561 B
Parani
Ufafanuzi
Parani ni jangwa lililopo mashariki mwa Misri na kusini mwa nchi ya Kanaani. Pia kulikuwa na mlima Parani ambalo yaweza kuwa jina lingine la mlima Sinai.
- Mtumwa Hagari na mtoto wake walikwenda kuishi katika jangwa la Parani baada ya Sara kumuamuru Abrahamu amfukuze.
- Musa alipowaongoza Waisraeli kutoka Misri walipitia jangwa la Parani.
- Ilikuwa toka Kadesh-barnea kupitia jangwa la Parani ambalo Musa aliwatuma wapelelezi kumi na mbili kupeleleza nchi ya Kanaani na kuleta ripoti.
- Jangwa la Sini lilikuwa kaskazini mwa Parani.