sw_tw/bible/names/obadiah.md

947 B

Obadia

Ufafanuzi

Obadia alikuwa nabii wa Agano la Kale aliye tabiri dhidi ya watu wa Edomu, waliyo kuwa wazao wa Esau. Pia palikuwa na wanaume wengine waliyo itwa Obadia katika Agano la Kale.

  • Kitabu cha Obadia ni kifupi katika Agano la Kale na kinaeleza unabii Obadia aliyo upokea kupitia maono kutoka kwa Mungu.
  • Sio wazi sana lini Obadia aliishi na kutabiri. Inawezekana kipindi cha utawala wa Yehoramu, Ahazia, Yoashi, na Athalia, mfalme wa Yuda. Nabii Danieli, Ezekieli, na Yeremia walikuwa wakitabiri kipindi hichi.
  • Obadia pia ina wezekana aliishi kipindi cha mwisho cha muda huu, wakati wa utawala wa Mfalme Zedekia na mateka ya Babiloni.
  • Wanaume wengine wa wenye jina Obadia ni mzao wa Sauli, Mgadi aliye kuwa mmoja wa wanaume wa Daudi; mtumishi wa hikulu wa Mfalme Ahabu; afisa wa Mfalme Yehoshafati; Mlawi aliye kuwa mlinzi wa lango kipindi cha Nehemia.
  • Ina weza kuwa mwandishi wa kitabu cha Obadia alikuwa mmoja wapo.