sw_tw/bible/names/kingdomofjudah.md

761 B

Yuda, ufalme wa Yuda

Ufafanuzi

Kabila la Yuda lilikuwa kubwa zaidi kati ya makabila kumi na mbili ya Israeli. Ufalme wa Yuda uliundwa na makanila ya Yuda na Benyamini.

Baada ya mfalme Sulemani kufa, taifa la Israeli liligawanyika katika falme mbili: Israeli na Yuda. Ufalme wa Yuda ulikuwa ufalme wa kusini, uliokuwa magharabi mwa Bahari ya Chumvi. Mji mkuu wa ufalme wa Yuda ulikuwa Yerusalemu. Wafalme wanane wa Yuda walimtii Yahwe na kuwaongoza watu kumwabudu yeye. Wafalme wengine wa Yuda walikuwa waovu na kuwaongoza watu kuabudu sanamu. Zaidi ya miaka 120 baada ya Ashuru kuishinda Israeli (ufalme wa kaskazini), Yuda ilitekwa na taifa la Babeli. Wababeli waliangamiza mji na hekalu, na kuwachukua watu wengi wa Yuda kwenda Babeli kama watekwa.