13 lines
601 B
Markdown
13 lines
601 B
Markdown
# Yoabu
|
|
|
|
## Ufafanuzi
|
|
|
|
Yoabu alikuwa kiongozi muhimu wa jeshi kwa mfalme Daudi katika utawala wake wote.
|
|
|
|
Kabla Daudi hajawa mfalme, Yoabu tayari alikuwa mmoja wa wafuasi wake waminifu.
|
|
Baadaye, wakati wa utawala wa Daudi kama mfalme wa Israeli, Yoabu alikuwa kamanda mkuu wa jeshi la mfalme Daudi.
|
|
Yoabu alikuwa pia mpwa wa mfalme Daudi kwa kuwa mama yake alikuwa mmoja wa madada zake Daudi.
|
|
Wakati mwana wa Daudi, Absalomu, alipomsaliti kwa kujaribu kuuchukua ufalme, Yoabu alimuua Absalomu ili kumlinda mfalme.
|
|
Yoabu alikuwa mpambanaji mwenye hima na aliua watu wengi waliokuwa maadui wa Israeli.
|
|
|