sw_tw/bible/names/jeroboam.md

1.2 KiB

Yeroboamu

Ufafanuzi

Yeroboamu mwana wa Nebati alikuwa mfalme wa kwanza wa ufalme wa kaskazini wa Israeli kati ya 900-910 K.K. Yeroboamu mwingine, mwana wa mfalme Yoashi, alitawala juu ya Israeli karibu miaka 120 baadaye.

Yahwe alimpa Yeroboamu mwana wa Nebati utabiri kwamba atakuwa mfalme baada ya Sulemani na kwamba atayatawala makabila kumi ya Israeli. Sulemani alipokufa, makabila kumi ya kaskazini mwa Israeli yalimkaidi mwana wa Sulemani, Rehoboamu na badala yake walimfanya Yeroboamu kuwa mfalme wao, wakimuacha Rehoboamu kama mfalme wa makabila mawili tu ya kusini, Yuda na Benyamini. Yeroboamu alikuwa mfalme muovu aliyewaongoza watu kutomuabudu Yahwe na badala yake aliweka sanamu kwa ajili yao kuabudu. Waflame wengine wote wa Israeli walifuata mfano wa Yeroboamu na walikuwa wafalme waovu kama yeye alivyokuwa. Karibu miaka 120 baadaye, mfalme mwingine Yeroboamu alianza kutawala ufalme wa kaskazini mwa Israeli. Yeroboamu huyu alikuwa mwana wa Yoashi na alikuwa muovu kama wafalme wengine wote waliopita wa Israeli walivyokuwa. Licha ya haya yote, Mungu alikuwa na huruma juu ya Israeli na kumsaidia huyu mfalme Yeroboamu kuongeza ardhi na kuimarisha mipaka ya eneo lao.