sw_tw/bible/names/cyrus.md

569 B

Koreshi

Ufafanuzi

Koreshi alikuwa mfalme wa Uajemi aliyetengeneza himaya ya Uajemi katika mwaka wa 550 Kabla ya Kristo kwa njia ya kutawala Kijeshi. Katika historia alijulikana kama Koreshi mkuu.

  • Mfalme Koreshi aliishinda Babeli na kusababisha kuachiwa kwa Waisraeli waliokuwa mateka huko.
  • Koreshi alijulikana kwa tabia yake ya tabia yake ya uvumilivu kwa watu wa taifa alilolishinda. Ukarimu wake kwa Wayahudi ukapelekea kujengwa upya kwa hekalu ya Yerusalemu baada ya kipindi cha mateka.
  • Koreshi alitawala katika kipindi cha Danieli, Ezra na Nehemia.