sw_tw/bible/names/caesar.md

15 lines
991 B
Markdown

# Kaisari
## Ufafanuzi
Neno "Kaisari" lilikuwa jina au jina la heshima lililotumika kwa watawala wengi wa Dola ya Rumi. Katika Biblia, hili neno linahusisha kwa tawala tatu tofauti tofauti.
* Mtawala wa kwanza wa Rumi alikuwa anaitwa Kaisari alikuwa "Kaisaria Agustino," ambaye alitawala katika kipindi ambacho Yesu alizaliwa.
* Kama miaka thelathini baadaye, katika kipindi wakati Yohana Mbatizaji alipokuwa akihubiri, Tiberia Kaisari alikuwa mtawala wa dola ya Rumi.
* Tibaria Kaisari Alikuwa bado anatawala Rumi wakati Yesu alipowaambia watu kumlipa Kaisari kile alichokuwa anastahili na kumpa Mungu alichokuwa anastahili.
* Wakati Paulo alipokata rufaa kwa Kaisari, hii ilimhusu mtawala mkuu wa Rumi, Neru, ambaye pia alikuwa na cheo "Kaisari"
* Wakati "Kaisari" linatumika lenyewe kama cheo, pia linaweza kutafsiriwa kama: "Dola" au "Utawala wa Rumi."
Katika majina kama Kaisari Agustino au Tiberia Kaisari, "Kaisari" inaweza kutamkwa karibia na vile lugha ya taifa inavolitamka.