sw_tw/bible/names/benjamin.md

452 B

Benjamini

Ufafanuzi

Benjamini alikuwa mwana wa mwisho wa Yakobo aliyezaliwa na Raheli mkewe. Jina lake linamaanisha mwana wa "mkono wangu wa kulia."

  • Yeye na Yusufu, nduguye mkubwa walikuwa wana pekee wa Raheli, aliyekufa baada ya kuzaliwa kwa Benjamini.
  • Wana wa Benjamini walikuwa mojawapo ya makabila ya Israeli.
  • Mfalme Sauli alikuwa akitokea katika kabila la Benjamini.
  • Mtume Paulo pia alikuwa wa kutoka katika kabila la Benjamini.