501 B
501 B
Baruku
Ufafanuzi
Baruku ni jina la watu kadhaa katika Agano la Kale.
- Baruku wa kwanza (mwana wa Zabeli) alifanya kazi ya Nehemia kujenga upya kuta za Yerusalemu.
- Lakini pia katika nyakati za Nehemia, Baruku mwingine (mwana wa Kol-Hoze) alikuwa miongoni mwa viongozi walioishi Yerusalemu baada ya kuta zake kujengwa.
- Baruku mwingine (mwana wa Neria) alikuwa mhudumu wa nabii Yeremia, kwa kumsaidia kazi mbalimbali kama vile kuandika jumbe Mungu alizompa Yeremia na kisha kuwasomea watu.