sw_tw/bible/names/balaam.md

13 lines
823 B
Markdown

# Balaamu
## Ufafanuzi
Balaamu alikuwa nabii wa kipagani aliyeajiriwa na Mfalme Balaki kuwalaani Israeli walipokuwa wamepiga kambi katika Mto Yordan kaskazini mwa Moabu, wakijiandaa kuingia nchi ya Kanaani.
* Balaamu alikuwa akitoka katika mji wa Pethori, ulikuwa katika eneo karibu na Mto Frati, umbali wa maili 400 kutoka katika nchi ya Moabu.
* Balaki, mfalme wa Wamidiani, alitishwa na nguvu na idadi ya Waisraeli, hivyo akamwajiri Balaamu kuwalaani.
* Kadiri Balaamu alivyosafiri kuwaelekea Israeli, malaika wa Mungu alisimama katika njia yake hivyo punda wa Balaamu alipomwona alisimama. Mungu akampa punda uweza wa kuongea na Balaamu.
* Mungu hakumuruhusu Balaamu kuwalaani Israeli badala yake alimwagiza kuwabariki.
* Baadaye, Balaamu bado alilete uovu juu ya Israeli alipowafuta kuabudu mungu wa Baar- peori.