sw_tw/bible/names/asherim.md

860 B

Ashera, sanamu ya ashera, Ashtorethi

Ufafanuzi

Ashera lilikuwa jina la mungu wa kike aliyeabuniwa na Wakaanani kipindi cha agano la kale. Ashtorethi ni jina lingine la Ashera.

  • Sanamu ya Ashera ni kinyago kilichochongwa kwa mbao au mti uliochongwa kwa ajili ya kumwakilisha mungu wa kike.
  • Sanamu za Ashera zilikuwa zinawekwa karibu na madhabahu za mungu Baali, aliyekuwa anadhaniwa kuwa mume wa Ashera. Watu wengine walikuwa wanamuabudu Baali kama mungu wa jua na Ashera kama mungu wa mwezi.
  • Mungu aliwaamuru Waisraeli wahaaribu vinyago vyote vilivyochongwa vya Ashera.
  • Baadhi ya Waisraeli kama Gideoni, mfalme Asia na mfalme Yosia walimtii Mungu na kuwaongoza watu kuharibu sanamu hizo.
  • Lakini viongozi wengine wa Israeli kama mfalme Solomoni, Mfalme Manase na mfalme Ahabu hawakuziharibu sanamu za Ashera na waliwashawishi watu waziabudu.