641 B
641 B
Asafu
Ufafanuzi
Asafu alikuwa kuhani wa Kilawi na mtaalamu wa muziki aliyetunga mziki wa Zaburi ya mfalme Daudi. Pia aliandika zaburi yake mwenyewe.
- Asafu alichaguliwa na mfalme Daudi kuwa moja ya wanamuziki watatu waliokuwa wakitengeneza nyimbo za kuabudu hekaluni. Baadhi ya nyimbo hizi zilikuwa unabii.
- Asafu aliwafundisha watoto wake na wakabeba majukumu ya kutumia vyombo vya muziki na kutoa unabii hekaluni.
- Baadhi ya vyombo vya mziki vilivyokuwepo ni kinanda, kinubi, tarumbeta na matoazi.
- Zaburi ya 50, 73-83 inasemekana zimetoka kwa Asafu. Na pia inawezekana baadhi ya zaburi hizi zimeandikwa na wanafamilia wake.