sw_tw/bible/names/absalom.md

703 B

Abusalomu

Ufafanuzi

Abusalomu alikuwa mtoto wa tatu wa mfalme Daudi. Alijulikana kwa utanashati wake pamoja na hasira kali.

  • Tamari Dada yake na Abusalomu alipobakwa na kaka yake Amnoni, Abusalomu alipanga mpango wa kumuua Amnoni.
  • Baada ya kumuua Amnoni, Abusalomu alikwenda mpaka mji ya Geshuri (mahali alipotokea Mika mama yake) na kuishi kule miaka mitatu. Kisha mfalme Daudi akaagiza arudi Yerusalemu, lakini hakumruhusu Abusalomu akaribie kwenye uwepo wake kwa miaka miwili.
  • Abusalomu aliwafanya baadhi ya watu kuwa kinyume na mfalme Daudi na kuwaongoza katika uasi dhidi ya mfalme.
  • Jeshi la Daudi lilipigana na Abusalomu na kumuua. Daudi alikuwa na huzuni sana yalipotokea haya.