sw_tw/bible/kt/zion.md

926 B

Sayuni, Mlima Sayuni

Ufafanuzi

Hapo awali, neno "Sayuni" au "Mlima Sayuni" lilimaanisha ngome ambayo Mfalme Daudi aliiteka kutoka kwa Wayebusi. Majina haya yakawa njia nyingine ya kuitaja Yerusalemu.

  • Mlima Sayuni na Mlima Moria ilikuwa milima miwili mji wa Yerusalemu ulipojengwa juu yake. Baadaye, "Sayuni" na "Mlima Sayuni" ikawa ikitumika kama maneno ya jumla kuitaja milima yote na mji wa Yerusalemu. Wakati mwingine pia yalitumika kutaja hekalu lililokuwako Yerualemu. (Tazama: [aina hii ya maana] (https://git.door43.org/Door43/en-ta-translate-vol2/src/master/content/figs_metonymy.md))
  • Daudi aliita Sayuni, au Yerusalemu, kama "Mji wa Daudi." Hii ni tofauti na mji wa alikozaliwa Daudi, Bethlehemu, ambao pia uliitwa Mji wa Daudi.
  • Neno "Sayuni" limetumika katika njia nyingine za tamathali za semi, kuitaja Israeli au Ufalme wa kiroho wa Mungu au katika mji mpya wa Yerusalemu atakaouanzisha Mungu.