sw_tw/bible/kt/zealous.md

879 B

kicho, uchaji

Ufafanuzi

Maneno "kicho" na "uchaji" yanamaanisha kujitoa kwa nguvu zote kumuunga mkono mtu au wazo.

  • Kicho inahusisha tamaa kubwa na matendo yanayoimiza jambo jema. Mara kwa mara inatumika kumwelezea mtu ambaye kwa uaminifu anamtii Mungu na kuwafundisha wengine kufanya hivyo pia.
  • Uchaji unahusisha kuweka bidii kubwa katika kufanya jambo na kuendelea katika bidii hiyo.
  • "Kicho cha Bwana" au "kicho cha Yahwe" yarejerea matendo ya Mungu yenye nguvu na endelevu katika kuwabariki watu wake au kuona haki ikitendeka.

Maoni ya Ufasiri

  • Kuwa "mchaji" yaweza pia kufasiriwa, "kuwa na bidii kubwa" au kufanya jitihada "zaidi."
  • Neno "kicho" laweza pia kufasiriwa kama "uchaji wa ndani" au "maamuzi ya kina" au "hamu ya haki."
  • Kirai, "kicho cha nyumba yako" yaweza kufasiriwa, "kuliheshimu sana hekalu lako" au "tamaa ya kuitunza nyumba yako."