sw_tw/bible/kt/yahweh.md

575 B

Yaweh

Ufafanuzi

Yaweh ni jina la Mungu alilolithihirisha alipozungumza na Musa katika kichaka kinachowaka moto.

  • Jina Yaweh linatokana na neno lenye maana ya "kuwepo."
  • Maana nyingine ya Yaweh ni "Niko" au "anayesababisha kuwepo."
  • Jina hili linadhihirisha kuwa Mungu alikuwepo na ataendelea kuishi daima. Pia inamaanisha kuwa yupo sasa.
  • Tafsiri nyingi za Biblia zimetumia neno "BWANA" kuwakilisha Yaweh. Biblia za kisasa zimeandika BWANA kwa herufi kubwa kuonesha heshima kwa jina la Mungu na kutofautisha na Bwana ambayo ilitumika katika maneno ya Kiebrania.