sw_tw/bible/kt/wordofgod.md

791 B

Neno la Mungu, Neno la Yaweh, Neno la Bwana, maandiko

Ufafanuzi

Katika Biblia neno la Mungu ni kitu chochote ambacho Mungu anawaambia wanadamu. Hii ni pamoja na lililoandikwa au kutamkwa. Yesu pia anaitwa "neno la Mungu.

  • "Maandiko" ni maandishi . Imetumika tuu katika agano jipya na imeelezea maandiko ya Kiebrania au agano la kale. Maandishi haya yalikuwa ujumbe toka kwa Mungu aliowaambia watu kuandika ili miaka ya baadae watu waweze kuyasoma.
  • Neno la Yaweh au neno la Bwana ni ujumbe toka kwa Mungu aliopewa nabii au mtu mwingine katika Biblia.
  • Mara nyingine neno hili hutokea kama "neno" au "neno langu" au "neno la Mungu.
  • Katika agano jipya Yesu anaitwa "neno" na "neno la Mungu." Cheo hiki kinamaanisha kuwa Yesu alidhihiridha Mungu ni nani kwa sababu yeye ni Mungu.