sw_tw/bible/kt/wise.md

583 B

Busara, hekima

Ufafanuzi

Busara inamuelezea mtu anayeelewa jambo la haki na mambo ya maadili na akayafanya. Hekima ni uelewa na kutenda yaliyo sahihi na maadili ya haki.

  • Kuwa na busara inajumuisha uwezo wa kufanya maamuzi mazuri hasa kuchagua kufanya yanayompendeza Mungu.
  • Katika Biblia "busara za dunia" inamaanisha kitu ambacho watu wa dunia wanafikiri ni burasa lakini ni upuuzi.
  • Watu huwa na busara wanapomsikiliza Mungu na kunyeyekea kutii mapenzi yake.
  • Mtu mwenye busara ataonesha matunda ya roho mtakatifu kwenye maisha yake kama furaha, upendo na uvumilivu.