sw_tw/bible/kt/redeem.md

755 B

kukomboa, ukombozi, mkombozi

Ufafanuzi

"Kukomboa" au "ukombozi" ni kununua kitu kilichokuwa kinamilikiwa hapo mwanzo au kilichochukuliwa mateka. "Mkombozi" ni mtu anayekikomboa kitu au mtu.

  • Mungu alitoa sheria kwa Waisraeli kuhusu kukomboa watu wau vitu.
  • Kwa mfano mtu anaweza kumkomboa mtu aliyekuwa utumwani kwa kumlipia kiasi ambacho mtumwa yule atakuwa huru.
  • Kama ardhi ya mtu imeuzwa, ndugu wa yule mtu anaweza kuikomboa au kuinunua tena ardhi ile ili ibaki kwenye familia.
  • Tendo hili linaonesha namna ambavyo Mungu aliwakomboa watu wake toka kwenye utumwa wa dhambi. Yesu alipokufa msalabani alilipia dhambi za watu nakukomboa watu wote wanaoamini ukombozi wake. Watu waliokombolewa na Mungu wapo huru toka kwenye dhambi na adhabu.