sw_tw/bible/kt/flesh.md

1.5 KiB

mwili

Ufafanuzi

Katika Biblia, msemo "mwili" una maana ya tishu laini ya mwili wa mwanadamu au mnyama.

Biblia pia hutumia msemo "mwili" kitamathali kumaanisha wanadamu wote au viumbe wote.

Katika Agano Jipya, msemo "mwili" unatumika kumaanisha asili ya dhambi ya wanadamu. Hii hutumika mara kwa mara kinyume na asili yao ya kiroho.

Msemo, "mwili na damu yake" ina maana ya mtu ambaye anahusiana kibiolojia na mtu mwingine, kama vile mzazi, ndugu, mtoto au mjukuu.

Msemo "mwili na damu" pia unaweza kumaanisha mababu au vizazi vya mtu.

Msemo "mwili mmoja" una maana ya muungano wa kimwili wa mwanamume na mwanamke katika ndoa.

Mapendekezo ya Tafsiri

Katika muktadha wa mwili wa mnyama, "mwili" unaweza kutafsiriwa kama "mwili" au "ngozi" au "nyama".

Inapotumika kumaanisha viumbe wote hai, msemo huu unaweza kutafsiriwa kama "viumbe hai" au "kila kitu chenye uhai".

Inapomaanisha kwa jumla watu wote, msemo huu unaweza kutafsiriwa kama "watu" au "binadamu" au "kila mtu anayeishi".

Msemo "mwili na damu" unaweza kutafsiriwa kama "jamaa" au "familia" au "ndugu wa karibu" au "ukoo wa familia". Kunaweza kuwa na muktadha ambapo inaweza kutafsiriwa kama "mababu" au "vizazi".

Baadhi ya lugha zinaweza kuwa na msemo ambao unafanana na "mwili na damu".

Msemo "kuwa mwili mmoja" unaweza kutafsiriwa kama "kuungana kimapenzi" au "kuwa kama mwili mmoja" au "kuwa kama mtu mmoja kimwili na roho". Tafsiri ya msemo huu unaweza kuangaliwa kuhakikisha inakubalika katika lugha na utamaduni wako.