677 B
677 B
Tohara
Ufafanuzi
Tohara ni kitendo cha kukata govi la mwanaume au mtoto wa kiume. Sherehe ya tohara hufanyika pamoja na tendo hili.
- Mungu alimuamuru Abrahamu awatahiri wanaume wote katika familia yake na watumishi wake kama ishara ya agano lao na Mungu.
- Mungu aliamuru uzao wa Abrahamu waendelee kufanya hivi kwa kila mtoto wa kiume katika nyumba hiyo.
- "Kutahiri moyo" ni mitendo cha kuondoa uovu wa mtu.
- Kwa namna ya kiroho "aliyetahiriwa" ni mtu ambaye ametakaswa na Mungu toka kwenye dhambi kupitia damu ya Yesu.
- "Wasiotairiwa" ni watu ambao hawajatahiriwa kimwili. Pia yaweza kuwa na maana ya ambao hawajatahiriwa kiroho wasiokuwa na mahusiano na Mungu.