sw_tw/bible/kt/christ.md

655 B

Kristo, Masihi

Ufafanuzi

Masihi na Kristo inamaana ya mpakwa mafuta na inamuelezea Yesu mwana wa Mungu.

  • Masihi na Kristo vimetumika katika agano jipya kumuelezea mwana wa Mungu ambaye Mungu baba alimpaka mafuta kutawala kama mfalme juu ya watu wake na kuwaokoa toka kwenye dhambi.
  • Katika agano la kale manabii waliandika unabii juu ya Masihi miaka mia kabla ya kuja kwake duniani.
  • Neno mpakwa mafuta limetumika katika agano la kale kumuelezea Masihi atakayekuja.
  • Yesu alitimiza unabii huo na alifanya miujiza mingi iliyothibitisha kuwa yeye ni Masihi, unabii uliobaki utatimia atakaporudi.
  • Neno Kristo hutumika kama jina "Kristo Yesu."