sw_tw/bible/kt/call.md

826 B

wito, kuita, ita

Ufafanuzi

wito, kuita ni kitendo cha kusema kitu kwa nguvu kwa mtu ambaye hayuko karibu. Pia kuna maana mbali mbali kama

  • Kuita mtu inamaana ya kupiga kelele au kuongea kwa sauti na mtu aliye mbali. Pia yaweza kuwa na maana ya kuomba msaada hasa kwa Mungu.
  • "wito" katika Biblia mara nyingi huwa na maana ya "kumwita" au "kuamuru aje" au "kumuomba aje."
  • Mungu huwaita watu kwake na kuwa watu wake. Huu ni wito wao.
  • Neno "kuitwa" limetumika kwenye Biblia kumaanisha kuwa Mungu aliwachagua au kuwateua watu kuwa watoto wake, watumishi wake na wasemaji wa ujumbe wa ukombozi kupitia Yesu.
  • Pia neno hili hutumika kwenye mukhtadha wa kumuita mju jina. Kwa mfano "Anaitwa Yohana," au "Jina lake ni Yohana."
  • "Nimekuita kwa jina lako" inamaana kuwa Mungu anafahamu jina la mtu na amemchagua yeye.