sw_tw/bible/kt/brother.md

1.7 KiB

ndugu

Ufafanuzi

Neno "ndugu" kwa kawaida linamaanisha ndugu wa kiume ambaye wanaunganishwa angalau na mzazi mmoja.

  • Katika Agano la Kale, neno "ndugu" lilitumika kama neno la taarifa ya jumla kwa ndugu, kama vile watu wa kabila moja, ukoo, au kikundi.
  • Katika Agano Jipya, mitume kwa kawaida walitumia "ndugu" kuwalejerea Wakristo wenzao, wakiwemo wa kike na wa kiume, kwa kuwa waumini wote katika Kristo ni washirika wa familia moja ya kiroho, wakiwa na Mungu kuwa Baba yao wa mbinguni.
  • Mara chache katika Agano Jipya, mitume kutumia neno "dada" wanaporejerea hasa kwa Mkristo mwenza aliyekuwa mwanamke, au katika kusisitiza kwamba wote wanaume na wanawake wanajumuishwa. Kwa mfano, Yakobo alisisitiza kwamba anazungumzia waumini wote anaporejerea "ndugu au dada aliye na mahitaji ya chakula au nguo."

Maoni ya Kutafasiri

  • Ni vema zaidi kutafasiri neno hili kwa neno halisi litumikalo katika lugha lengwa kurejerea kwa ndugu wa kibayolojia, isipokuwa neno hili linatoa maana potofu.
  • Katika Agano la Kale hasa, neno"ndugu" linapotumika kwa ujumla sana kurejerea watu wa familia moja, ukoo, au kikundi, maana pendekezwa ni pamoja na "ndugu" au "wanaukoo" au "Waisraeli wenzao."
  • Katika mazingira ya kurejerea kwa washiriki wenzao katika Kristo, neno hili liliweza kutafasiriwa kama, "ngugu katika Kristo" au "ndugu wa kiroho."
  • Ikiwa wote, wanaume na wanawake wametajwa na "ndugu" lingetoa maana potofu, hivyo neno la jumla zaidi la kindugu lingetumika ili kuwahusishawa wote wanaume na wanawake.
  • Njia nyingine ya kutafasiri neno hili ili kuwahusisha waumini wote wa kiume na wa kike lingekuwa, "waumini wenzao" au "Wakristo wa kike na wa kiume."
  • Hakikisha unaangalia mazingira kuamua kwamba ni wanaume pekee wametajwa, au kwamba wote wamehusishwa.