sw_tw/bible/kt/bornagain.md

1.2 KiB

Kuzaliwa upya, kuzaliwa na Mungu, kuzaliwa kwa roho

Ufafanuzi

Neno "kuzaliwa upya" lilitumiwa mara ya kwanza na Yesu kuelezea maana ya Mungu kumbadilisha mtu kutoka kuwa mfu kiroho na kuwa hai kiroho. Neno "kuzaliwa na Mungu" na "kuzaliwa kwa roho" pia hurejerea hali ya mtu kupewa uzima mpya kiroho.

  • Watu wote wanazaliwa wafu kiroho na wanapewa "kuzaliwa upya" wanapomwamini Yesu Kristo kama mwokozi wao.
  • Katika wakati wa kuzaliwa upya kiroho, Roho wa Mungu uanza kuishi ndani ya muumini mpya na kumtia nguvu ili azae matunda mema ya kiroho katika maisha yake.
  • Ni kazi ya Mungu kumfanya mtu kuzaliwa upya na kuwa mwana wake.

Maoni ya Tafasiri

  • Njia nyingine ya kutafasiri "kuzaliwa tena" inahusisha, "kuzaliwa upya" au "kuzaliwa kiroho."
  • Ni vizuri kutafasiri neno hili katika maana ya kawaida na kutumia neno la kawaida katika lugha litumikalo kwa kuzaliwa.
  • Neno "uzao mpya" laweza kutafasiriwa kama "kuzaliwa kiroho."
  • Kirai "liyezaliwa na Mungu" laweza kutafasiriwa kama "kufanywa na Mungu kuwa na uzima mpya kama mtoto aliyezaliwa upya au "kupewa uzima mpya na Mungu."
  • Kwa njia ileile, "amewezeshwa na Roho Mtakatifu kuwa mtoto wa Mungu" au "kufanywa na Roho kuwa na uzima mpya kama mtoto mchanga."