sw_tw/bible/kt/blasphemy.md

845 B

Kumkufuru

Ufafanuzi

Katika Biblia, neno "kufuru" inamaanisha kuzungumza kwa njia ambayo inaonesha dharau kubwa kwa Mungu au watu. "Kumkufuru" mtu ni kuongea kinyume cha mtu huyo ili watu wafikiri vibaya juu ya mtu huyo.

  • Mara nyingi, kumkufuru Mungu humaanisha kumtukana kwa kusema mambo ambayo siyo kweli kuhusu yeye au kwa kuenenda kwa njia isiyo na maadili hata kumvunjia heshima.
  • Ni kufuru kwa mwanadamu kudai kuwa Mungu au kudai kwamba kuna Mungu mwingine zaidi ya Mungu wa kweli.
  • Baadhi ya matoleo mengine yanatafasiri neno hili kama "kumtukana" linaporejerea kuwakufuru watu.

Maoni ya Tafasiri

  • "Kukufuru" kwaweza kutafasiriwa kama, "kusema vibaya dhidi ya" au "kumdharau Mungu" au "kumtukana".
  • Jinsi ya kutafasiri "kufuru" ni pamoja na. "kusema vibaya kuhusu wengine" au "kutukana" au "kusambaza tetesi za uongo."