sw_tw/bible/kt/antichrist.md

597 B

Mpinga Kristo

Ufafanuzi

"Mpinga Kristo" linamaanisha mtu au mafundisho ambayo ni kinyume na Yesu Kristo na kazi zake. Wapo wapinga Kristo wengi sana duniani.

  • Mtume Yohana anaandika kwamba mtu anaweza kuwa mpinga Kristo pale anapowapotosha watu kwa kuwaambia kuwa Yesu sio Masihi na kukataa kuwa Yesu ni Mungu.
  • Biblia pia inatufundisha kuwa kuna roho ya mpinga Kristo duniani ambayo inapinga kazi za Mungu.
  • Kitabu cha ufunuo kinaeleza kuwa kutakuwa na mtu atakayeitwa "mpinga Kristo" atakayejidhihirisha siku za mwisho. mtu huyu atajaribu kuwaangamiza watu wa Mungu Yesu atamshinda.