sw_tw/bible/kt/angel.md

986 B

Malaika, Malaika mkuu

Ufafanuzi

Malaika ni kiumbe chenye roho na chenye nguvu kilichoumbwa na Mungu. Malaika wanamtumikia Mungu kwa kufanya yale wanayoagizwa kuyafanya na Mungu. Malaika mkuu ni malaika anayewaongoza malaika wengine.

  • Malaika maana yake ni mjumbe.
  • Malaika mkuu maana yake ni mjumbe mkuu. Malaika pekee kwenye Biblia anayesemwa kama malaika mkuu ni Mikaeli.
  • Katika Biblia malaika wanafikisha ujumbe kwa watu toka kwa Mungu. Ujimbe huu ni pamoja na maelekezo juu ya nini Mungu anataka watu wafanye.
  • Malaika pia waliwaambia watu mambo yajayo.
  • Malaika wana mamlaka ya Mungu katika kumuwakilisha na wakati mwingine kwenye Biblia wamezungumza kama vile Mungu anazungumza.
  • Njia nyingine ambazo Malaika wanamtumikia Mungu nu kwa kuwalinda na kuwapa watu nguvu.
  • Malaika wa Yahweh ina maana mbili 1) "malaika wanaomwakilisha Yahweh" au "wajumbe wanaomtumikia Yahweh." 2) Yaweza kuwa na maana ya Yahweh mwenyewe aliyeonekana kama malaika alipoongea na mtu.