sw_tw/bible/kt/altar.md

472 B

Madhabahu

Ufafanuzi

Madhabahu ilikuwa sehemu yenye muundo ulioinuka ambao wana wa Israeli walichoma wanyama na mazao kama sadaka kwa Mungu.

  • Katika nyakati za Biblia madhabahu rahisi zilikuwa zinatengenezwa kwa kilima chenye udongo au mawe makubwa yaliyopangwa na kupafanya pawe imara.
  • Madhabahu nyingine zilitengenezwa kwa mbao pamoja na dhahabu na shaba.
  • Watu wengine walioishi karibu na Israeli walitengeneza pia madhabahu na kutoa sadaka kwa miungu yao.